Utajuaje kama unadanganywa?


Kiufupi nilikuwa ktk mahusiano na mdada mwanzoni tulipendana sana nilijitolea kwa mengi katika umoja wetu. Sasa alianza kubadilika kitabia kiujumla akawa hanijali, msili, hana muda na mimi, ahitaji ushirikiano na mimi.


Ikafika kipindi nikaanza kuhisi nasalitiwa lakiji nilimvumilia. Sasa nahitaji kujua je huyu Dada ni mkweli kwangu na ananipenda au? maana kuwa karibu na mimi imekuwa shida au tunakuwa tunagombna sana. Nikiwa nahitaji kujua kitu kuhusu yeye lazima tuishie kugombana. Sasa hivi imefika mwaka tupo kwenye mahusiano lakini simuelewi.

Sijawahi kufanya nae mapenzi nae nahisi hiyo ndio sababu ya kufanya haya yote na aliniambia yeye ni Bikra. Pia napenda kujua sifa za Bikra au utatambuaje msichana ulienae ni Bikra au la! na utajuaje kuwa unadanganywa au la!

***********


Dinah anasema: Hello there. Ahante kwa ushirikiano.

Umri wa uhusiano wenu ni mdogo sana kujua kama mtu kabadilika. Nadhani hajabadilika isipokuwa hana hisia alizokuwa nazo kwako mlipoamua kuwa pamoja. Nimeondoa sehemu ya maelezo yako ili kukuachia a bit of privacy. Umri wa binti huyo ni mdogo kwa yeye kujua atakacho kutokankwenye uhusiano. Bado yupo kwenye kipindi cha mpito cha kujifunza ujinsia wake.


Anapata hisia za kutaka kuwa karibu na mwanaume na kuna kuwa na wengi wanavutiwa nae na hivyo anashindwa kujua wapjnpa kwenda na ku commite......hii haina maana kuwa analala nao la hasha....bali wanakuwa kichwani na hivyo kumhuia vigumu kufanya uamuzi.

Wanaume wengi kumtaka inampa hali ya kujiamini na haoni tatizo kuachana na wewe kwani kuna foleni. Sasa unapokuwa too demanding na kuanza ku act as if umemuoa au kama Baba au Kaka yake ndio matatizo yanapoibuka.


Anahitaji kuwa huru anapokuwa nje ya nyumbani ambako kuna wafuatiliaji (Baba na Kaka)......sasa kama hapati uhuru kutoka kwako ni wazi atatafuta namna ya kuachana na wewe. Kama bado unataka kuwa na uhusiano huu basi unahitaji kubadilika......badilisha tabia yako ya kuwa too demanding na ku act kama mume kwake wakati sio mume na pengine hutokuwa mume wake.



Sidhani kama kuyofanya nae mapenzi ndio sababu ya yeye kuwa hivyo alivyo. Nadhani tabia zako kwake ndio zinamsogeza mbali nawe. Kuwa mpenzi na sio Baba au kaka.....punguza maswali na upunguze kumfuatilia. Kujua kama mtu anakudanganya ni rahisi ikiwa unajua kuitumia sixth sense yako. Pia kama umeishi na mtu huyo kwa muda ambao ni zaidi ya miaka 2. Hii ni kwasababu mtu unaeishi nae hawezi kuigiza kwa miaka 3.....lazima atachoka na kuvua Wasifu.



Baadhi ya watu huingiza kwa muda mrefu ili kupata watakacho au zaidi mpaka wakaipate. Utamjuaje kama ni Bikira? Well hakuna njia zaidi ya kumuamijk kuwa hajawahi kushiriki tendo. Siku ya siku ikifika rudi kwangu uniamjie ilivyokuwa then nitakuambia kama ni mara ya kwanza kwake au siku ya kwanza na wewe.


Nia na madhumuni ya Uhusiano wa kimapenzi ni kukubalibali kuwa na mtu umpendae na kufurahia umoja wenu. Ikiwa kwenye umoja huo hakuna furaha na unadhani hakuna namna ya kuipata furaha baada ya mazunhumzo na mabadilikonkadhaa basi ni vema kutoka na kuanza upya.

Kila la kheri.

Comments